Pages

Monday, July 5, 2010

UCHEKI MLIMA WENYEWE KWA POZI HILI TENA!!!!!!!

JAMANI MLIMA WETU WA KILIMANJARO MZURI!!!!!!!!!!!!!!!!!!

ILI TANZANIA ICHUKUE KOMBE LA DUNIA INABIDI UWANJA UWE HIVI!!!

Rais Kabila wa Kongo atangaza siku mbili za maombolezo

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ametangaza siku mbili za maombolezo, baada ya watu 235 kupoteza maisha yao katika moto. Ajali hiyo ilitokea baada ya lori lililopakia mafuta kupinduka

na kuripuka katika Wilaya ya Kivu ya Kusini.



Moto huo, ulienea katika jengo ambako watu walikuwa wakitazama mchezo wa Kombe la Dunia. Watu wengine walikufa walipokuwa wakichota mafuta katika lori hilo. Umoja wa Mataifa pia umesema kuwa wanajeshi wake 5 wa vikosi vya amani walipoteza maisha yao walipokuwa wakiwazuia watu kukaribia lori hilo.

Comments
Add New Search

Masheikh wasusia ripoti mahakama ya kadhi

RIPOTI ya kwanza kuhusu mapendekezo ya sekretarieti ya pamoja kati ya wataalamu wa serikali na wa kiislaam, juu ya mfumo na uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara, imekwaa 'kisiki'.

Hatua hiyo imekuja baada ya jopo la masheikh 25, likiongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa bin Shaaban Simba, kuikataa kwa maelezo kuwa ina mapungufu.

Hivi karibuni Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mufti Simba kwa nyakati tofauti, waliwaambia waandishi wa habari kuwa Mahakama ya Kadhi, iko jikoni na kwamba muda si mrefu, itaiva.

Viongozi hao waliwasihi Waislaam kote nchini, wasiwe na wasi wasi.
Hata hivyo juzi Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam (T) na Shura ya Maimamu, yalisema kupitia katika tamko yao kwamba hawataikubali mahakama itakayoundwa, ikiwa haitatambuliwa kikatiba na kutengewa bajeti na serikali.

Kufuatia kauli hizo na ile ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoweka bayana kwamba haitaiingiza tena hoja ya Mahakama ya Kadhi katika ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2010/15, jopo la masheikh lilitisha kikao cha siku mbili chini ya Mufti Simba, kujadili ripoti ya kwanza ya mapendekezo ya mfumo na uendeshaji wa mahakama hiyo.

Kikao hicho kilichoanza Julai 3 na kumalizika Julai 4 mwaka huu, kilijadili kipengele kwa kipengele ripoti hiyo na kugundua kuwa ilikuwa na mapungufu makubwa kuhusu mambo muhimu ya mahakama hiyo inayoliliwa na Waislaam kwa miaka 20 sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Katika Makao Makuu ya Bakwata jijini Dar es Salaam jana, mufti Simba, alisema jopo limebaini kuwa, kuna mambo muhimu yanayohitaji kujadiliwa tena kati ya serikali na Waislamu.

"Jopo limekaa na kujadili kipengele kwa kipengele na kuona kwamba bodo kuna mambo muhimu ambayo yanahitaji kukaa tena na serikali ili kufikia mwafaka," alisema mufti Simba.

Mufti Simba alisema mambo hayo yanahusu mfumo wa uendeshwaji wa mahakama na kwamba , jopo halikukubaliana na mfumo uliopendekezwa katika ripoti hiyo.

"Kwanza ni vipi mahakama ya kadhi itakuwa na uwezo wa kisheria na kikatiba wa kutoa maamuzi yake, pili ni vipi mahakama itaingizwa katika mfumo wa mahakama uliopo nchini na namna ya kugharamia uendeshwaji wake,"alisema mufti Simba.

Hata hivyo Mufti Simba ambaye ni msemaji wa jopo hilo la kufuatilia mchakato wa urejeshwaji wa Mahakama ya Kadhi Tanzania bara, aliwataka Waislaam na watu wa madhehebu mengine nchini,kuwa watulivu.

"Tunaomba Waislaam na wananchi wote kwa jumla kuwa, watulivu kwa kuwa jambo hili ni zito na linahitaji umakini wa hali ya juu katika kufikia mwafaka," alisema.

Alisema jopo limepokea mapendekezo yaliyofikiwa kati ya Sekretarieti ya Serikali na Waislaam, kuhusu namna ya kuunda na kuendesha mahakama hiyo.
.
Alisema kikao hicho kimepata mahudhurio mazuri kwa kuhudhuriwa na wajumbe wote 25 kutoka taasisi na madhehebu mbalimbali ya kiislaam pamoja na wanasheria (mawakili).

Aliwataja wajumbe kuwa ni, masheikh Issa bin Shaaban Simba (Mwenyekiti), Salum Hassan Fereji (Bakwata), Ally Muhidini Mkoyogore (Bakwata), Ismail Makusanya (Bakwata), Shaban Rashid (Bakwata), Abdillahi Mnyasi (Bakwata) na Abubakar Zubeir (Salafia).

Wengine ni masheikh Hamid Jongo (Bakwata), Alhad Mussa Salum (Bakwata), Muhammed Jalal Sharif (Daawatil Islaamiyya), Ramadhan Lakha (Sunni), Mussa Kundecha (Baraza Kuu), Suleiman Kilemile (Masjid Thaqafa), Muharrami Dogga (Alharamain) na Twaha Selemani Bane (Alharamain).

Masheikh wengine ni, Juma Omar Porri (Answar Sunna), Abdallah Bawazir (Qiblatain), Twalib Ahmad Abdallah (Masjid Maamur), Abdallah Ndauga (I.I.R.O), Said el-Maamriy (wakili), Issa Maige (wakili), Yahya Njama (wakili), Mohammed Khamis Said (Bakwata), Abdallah Matumla (Mwanasheria Bakwata) na Suleiman Lolila (Bakwata).

Hata hivyo Mufti Simba alisema hana uhakika kama serikali itaendelea kulitekeleza la mahakama ya kadhi baada ya uchaguzi iwapo halikumalizika kwa sasa.

CHANZO MWANANCHI

Polisi ajiua kwa kuupoteza msafara wa Rais Kikwete,AJIPIGA RISASI AKIWA RUMANDE

SAA chache tu baada ya msafara wa Rais Jakaya Kikwete, kuingia katika Kanisa a Anglikana, ili kuhudhuria sherehe za kuwekwa wakfu Askofu, askari polisi wa kike WP Suzana, amejiua kwa kujipiga risasi baada ya kuwekwa mahabusu kwa kosa la kuupoteza njia, msafara wa Rais.

Habari zilisema tukio hilo lililogeuka kuwa gumzo katika mji huo, lilitokea saa 8 mchana wa jana, katika Kituo cha Polisi Tarime, muda mfupi baada ya askari huyo kuwekwa chini ya ulinzi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Dk Charles Samson, alikiri kuupokea mwili wa askari huyo na kwamba alijipiga risasi upande wa kushoto wa kifua.

Kwa mujibu wa Mganga huyo, risasi hiyo ilipenya na kutokea nyuma ya bega.

"Ni kweli amejiua kwa kujipiga risasi ambayo imetokea nyuma ya bega. Kwa ufupi ni kwamba eneo hilo ni sehemu ya moyo, nimemfanyia uchunguzi wa awali na
kuthibitisha kuwa amekufa,"alisema.

Alisema taarifa kuhusu tukio hilo alizipata akiwa katika msafara wa Rais na kwamba alipokwenda kumfanyia uchunguzi marehemu, alibaini kuwa alikata roho muda mfupi,baada ya kujipiga risasi.

"Kitaalam kilichosabaisha kifo ni risasi maana nimefanya uchunguzi na kubaini, nasubiri uchunguzi mkubwa tukiwa na polisi ili tuwakabidhi maiti kwa ajili ya hatua nyingine,"alisema kwa masikitiko.

"Sijui nini kimempelekea kujiua maana huo ni uamuzi mzito sana aliochukua," alisisitiza Mganga mkuu.

Kwa upande wake, mhudumu wa chumba cha maiti katika hospitali hiyo, Samweli Malindi, alisema marehemu alifikishwa katika katika chumba hicho kwa kutumia gari la polisi.

"Walisema amejiua kwa sababu ya kuongoza vibaya msafara wa Rais na kuwekwa mahabusu," alisema.

Chanzo kimoja cha uhakika kutoka ndani ya jeshi hilo, kililiambia
gazeti hili kuwa kiini cha askari huyo kujiua ni kuwekwa mahabusu huku akitishiwa kuchukuliwa hatua kali zaidi.

Chanzo hicho kilisema msafara wa Rais ulitakiwa kuingia kwa mkuu wa wilaya, kabla ya kwenda kanisani, lakini yeye aliruhusu magari kwenda moja kwa moja na gari la Rais likielekea kwa mkuu wa wilaya, jambo lililosababisha safara ukagawanyika na baadaye kulazimika kurudi.

"Kitendo hicho kiliwachukiza viongozi na kuamuru kukamatwa na kuwekwa
mahabusu kwa askari huyo. Wakati akiwa mapokezi ghafla alichukua bunduki aina ya SMG na kujimiminia risasi tatu na kukata roho papo hapo," kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilidai kuwa askari huyo ni miongoni mwa askari polisi waliotoka chuoni hivi karibuni na kwa hiyo si mzoefu.
Chanzo hicho kilisema katika hali ya kawaida viongozi walipaswa kumsaidia kwa kutumia lugha ambayo vinginevyo isingemfanya ajisikie vibaya na kuchukua uamuzi huo. Baadhi ya wananchi wakizungumza na Mwananchi walisema hayo ni matatizo ya matumizi ya nguvu ndani ya jeshi.

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Polisi ya Tarime/Rorya, Constantine Masawe,alisema alikuwa nje ya ofisi."Niko Dar es Salaam na wala sikuwa na taarifa, amejiua kwa nini, maana sijaambiwa,"alisema.

Rais Kikwete, alikuwa amekwenda Tarime kuhudhuria kuwekwa wakfu kwa Askofu Dk Mwita Akiri.

CHANZO MWANANCHI

Urais Zanzibar: Raza, Karume wawa mbogo

Wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar wamesema hawaamini kama Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM, imependekeza wagombea watano tu kuwa wanafaa kuteuliwa kuwania urais wa visiwa hivyo.
Wamesema ikiwa mapendekezo hayo yametolewa itakuwa ni kinyume cha utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wagombea hao, Balozi Ali Karume na mfanyabiashara maarufu, Mohammed Raza, ni miongoni mwa wana-CCM 11 wanaoomba ridhaa ya chama hicho kugombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Waliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika mdahalo wa wagombea wa urais wa Zanzibar kupitia CCM uliofanyika jana kisiwani hapa na kudhaminiwa kwa ushirikiano wa kampuni za Vox Media na ASAM-PR.
Balozi Karume alisema kama CCM-Zanzibar imependekeza majina matano yaliyochapishwa jana katika vyombo vya habari, itakuwa imekwenda kinyume cha utaratibu wake na kwamba suala la kuwekewa alama lilishafutwa.
“Siamini kama kuna wagombea wamependekezwa, inawezekana maneno ya magazeti na kama ni kweli, basi tulipaswa kuambiwa wamepatikana kwa utaratibu gani, kama wamepigiwa kura au wameteuliwa,” alisema Balozi Karume ambaye ni mdogo wake Rais Amani Karume wa Zanzibar aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM visiwani hapa iliyopitia majina ya wagombea hao juzi.
Hata hivyo, alisema anaamini majina ya wagombea wote yatakwenda Dodoma, kwa vile kikao cha Zanzibar kinawajibika katika kuwajadili wagombea, kabla ya Kamati Kuu kuchagua majina matatu ya kupeleka Halmshauri Kuu ya Taifa (Nec) kwa ajili ya kupitisha jina moja la mgombea urais wa Zanzibar.
CCM ilifuta utaratibu wa wagombea wa nafasi hiyo kupigiwa kura Zanzibar na kuwekewa alama, baada ya matatizo yaliyojitokeza katika mchakato wa mwaka 2000 na 2005.
Kwa upande wake, Raza alielezea kushangazwa na taarifa kwamba majina matano ya wagombea, yalipendekezwa katika kikao cha kamati hiyo, bila kuelezwa utaratibu uliotumika na kuwapata wagombea hao.
“Bado siamini kama kuna wagombea bora wamependekezwa, nipo tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayotolewa na chama changu,” alisema Raza.
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhani Ferouz, alisema maamuzi yote yaliopendekezwa katika kikao hicho, yataendelea kubakia siri hadi yatakapowasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu.
“Si kila tunachokiamua kielezwe katika vyombo vya habari, CCM ina taratibu zake za kuendesha vikao na mapendekezo yalitolewa na kikao yataendelea kubakia siri hadi yatakapowasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu,” alisema.
Naibu Katibu huyo alisema hayo baada ya kutakiwa na Nipashe jana, kufafanua utaratibu uliotumika katika kuwapata wagombea hao watano.
Habari kutoka ndani ya CCM ziliwataja wagombea watano waliopendekezwa kuwa wanafaa kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar ni Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk. Mohamed Gharibu Bilal, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna, Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman.
Wagombea wengine kati ya hao 11 waliojitosa kwenye kinyang’anyiro mbali na Naibu Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mohammed Aboud, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Hamad Bakari Mshindo, Muhamad Yussuf Mshamba, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Omar Sheha Mussa.
Wakati huo huo, wagombea nafasi ya urais wa Zanzibar wawili tu, waliojitokeza katika mdahalo kati ya wagombea 11 wanaoomba kuteuliwa na CCM kuwania nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa mdahalo huo, Ali Saleh, alisema wagombea wote walipewa mialiko mapema, lakini wagombea watatu tu ndio walitoa sababu za kutohudhuria, baada ya kutingwa na ratiba nyingine za kazi.
Aliwataja wagombea waliotoa sababu za kutohudhuria kuwa ni Suleiman, Mshindo na Nahodha ambaye anahudhuria vikao vya bajeti ya mwaka wa fedha 2010/2011
“Tunashukuru kuweka historia kwa kuwakutanisha wagombea wa nafasi nyeti kama hii, pamoja na kuwa wagombea wengine wameshindwa kuhudhuria na kuwanyima haki wananchi wa Zanzibar, ya kutaka kufahamu kwa nini wanaomba ridhaa ya kupewa Urais,” alisema.
Kwa upande mwingine, Balozi Karume alisema ikiwa atafanikiwa kuwa Rais, ataijenga misingi mizuri ya kisiasa na kiuchumi, kwa kuimarisha sekta ya elimu ili kuongeza ajira kwa vijana na kuimarisha kiwango cha ubora wa elimu.
Pia alisema hatasita kusaini adhabu ya kifo kwa kwa mtu yeyote iwapo taratibu za kisheria zitazingatiwa kwa mujibu wa sheria.
Balozi Karume alishangazwa na Zanzibar kutoruhusiwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), badala yake kuruhusiwa nchi za Ruwanda na Burundi kwa madai kuwa mataifa hayo, yalikuwa sehemu ya Tanganyika kabla ya mgawanyo wa mipaka wakati wa ukoloni.
“Rwanda na Burundi ni nchi zilizokuwa sehemu ya Tanganyika, inakuwaje ziruhusiwe kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Zanzibar inyimwe,” alihoji.
Naye Raza alisema utatuzi wa kero za Muungano ni sehemu ya vipaumbele vyake ikiwa atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar.
Kamati Kuu ya CCM inatarajiwa kuwajadili wagombea nafasi ya urais wa Zanzibar wiki hii, kabla ya kupendekeza majina matatu katika kikao cha Nec kitakachochagua mgombea urais wa Zanzibar Julai 9 mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE

World Cup 2010 - Cristiano Ronaldo becomes a father - Yahoo! Eurosport

World Cup 2010 - Cristiano Ronaldo becomes a father - Yahoo! Eurosport

Joseph Pastor Lyaruu Kugombea Udiwani Kata ya Kilema Kati kupitia CHADEMA


Mwalimu na mkulima wa siku nyingi toka Kijiji cha Immi Kata ya Kilema Kati Ndugu Joseph Pastor Lyaruu, ametangaza nia ya kugombea udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA katika uchaguzi mkuu utakao fanyika baadae mwaka huu. Akizungumza na blog hii Ndugu Joseph ameweka hadharani baadhi ya vipaumbele vyake endapo atateuliwa kugombea kupita CHADEMA na kushinda uchaguzi huo hapo baadae mwaka huu. Miongoni mwa vipau mbele vyake ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanaondokana na kilimo cha mazoea na kuongeza tija kwenye kilimo. Pia amesema atahakikisha anavutia wawekezaji wa hoteli za kitalii pamoja na kuhamasisha utalii katika eneo la Kilema hususani utalii wa ikolojia. Pia amesema atashirikiana na wadau wengine kuongoza kampeni ya kuhifadhi mazingira na kuomba majengo ya kale yaliyoko Kilema kuingizwa katika maeneo nyeti ya uridhi wa dunia kupitia shirika la umoja wa mataifa la UNESCO.

Friday, July 2, 2010

Uchaguzi 2010 na Maendeleo ya Kilema

Hello wadau wa maendeleo ya Kilema.

Kama mjuavyo mwaka huu ni mwaka uchaguzi na kila ukipita maeneo ya Tanzania suala kubwa ni juu ya tukio hilo muhimu katika nchi yetu. Wakati mkiendelea kutafakari na kuwaza juu ya uchaguzi huo.. nimeona leo niwaletee swali la Je ni aina gani ya mtu anafaa kuwa Mbunge wetu na Diwani wetu katika Kilema? Jambo hili ni muhimu kwani kama mjuavyo maendeleo yetu yatapatikana tu iwapo tuna uongozi thabiti wenye uelewa wa mambo na ambao unaweza kukabiliana na changamoto za zama tulizopo na sio uongozi unaotaka kuendesha mambo kwa Mazoea.